Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Abdallah Mohamed ‘Baresi” amesema kuwa ameanza kufanyia kazi makosa waliyofanya washambuliaji wake katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu.

Mashujaa wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi tisa huku wakiwa wamefunga mabao sita na kufungwa 10.

Kocha Baresi amesema kuwa licha ya kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo iliyopita bado safu yake ya ushambuliaji haijamshawishi, ndio maana hivi sasa ameamua kuwapa mazoezi maalumnu kabla ya kurejea kwenye michezo ya ligi.

“Mechi za mzunguko wa pili ni ngumu tunataka kuanza kupunguza makosa yetu sio jambo rahisi nimeanza kuwaandaa wachezaji wangu wajipange tunaenda kukutana na upinzani mkubwa kwani kila timu itakuwa inahitaji kupata matokeo mazuri,

“Nimeiangalia safu yangu ya ushambuliaji haikuwa inafanya vizuri ndio maana nimeongezewa nyota wapya na wazoefu na Ligi Kuu Bara ambao naamini wanakuja kurudisha makali yetu kwenye eneo la ushambuliaji.” amesema Baresi.

Amesema kuwa kikosi chake kinaendelea vizuri japokuwa kuna mapungufu machache katika safu ya ushambuliaji ambayo hivi sasa ameanza kuifanyia kazi changamoto hiyo.

Wakimbizi wameteuliwa nafasi zenye maamuzi - Jenerali Mkunda
Chukueni tahadhari za kiafya wakati wa Mvua - Dkt. Haonga