Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaasa Wana- CCM kuendelea kueneza upendo, nidhamu na unyenyekevu ndani na nje ya chama na kwamba hawawezi kususa kuzungumza na vyama vya Wapinzani kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na Babab mwenye nyumba kususia Mboga.

Dkt. Nchimbi ametoa wito huo hii leo Januari 22, 2023 katika mapokezi yake Makao makuu ya CCM Jijini Dodoma ambapo amesema, amepewa heshima kubwa na Rais Samia kwa kuteuliwa hivyo upendo, amani na unyenyekevu viendelee kutawala na kwamba japo CCM ina nguvu lakini haiwezi kuwadharau wapinzani kwani ujenzi wa nchi ni wa wote.

Amesema, “hata kama tunaenda kushinda kwa kishindo lazima hatutokubali kuwa na kiburi bado tunatakiwa kuwa wanyenyekevu kwa vyama pinzani tuna Serikali inayojitambua, inayowajibika yenye Raisi mwenye upendo, kwahiyo tusilewe uongozi ambao tunao, lazima tuwe na nidhamu, tuepuke kiburi.”

Katika mapokezi hayo, aliyewahi kuwa Mbunge na Mweka Hazina wa CHADEMA Kanda, Upendo Peneza amekaribishwa rasmi katika Chama cha Mapinduzi ambapo amesema kwa muda mrefu amekuwa akivumilia vitendo vya ajabu vinavyofanyika katika chama pinzani, akiambatana na Ben Andrew aliyewai kuwa mwenyekiti wa Vijana CHADEMA Jimbo la Mbulu pamoja na Onesphor aliyewaikuwa katibu wa Chama chadema wilaya ya Morogoro..

“Wamefanya Biashara ya ulaghai kwa muda mrefu , kwaio wameshtuka tunakaribia uchaguzi, hivyo wanaanza kujisafisha taratibu mpaka tutakapofikia uchaguzi, na nmesikia Freeman Mbowe amefungua maandamano, kwa mawazo yangu tu maandamano hayo wanafanya ili kuangalia bidhaa ambazo wamebaki nazo na ambazo zimeondoka,” amesema Peneza

Ihefu kutumia uchochoro ASFC
Mwamba kukiwasha AFCON 2023