Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Mwanaada Kilima amesema Mtoto ametolewa Skrubu kwenye mapafu kwa kutumia kifaa chenye Kamera na kwenda kuinasa ambayo alikua akiichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka.

Mtoto huyo, alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida, ambapo mzazi wa mtoto huyo, Msafiri Chatanda amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.

Katikati ya mwezi huu, Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, pia lilifanikiwa kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto (5).

Aidha, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake pia walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye Kamera.

Hakuna nchi itakayoachwa nyuma - Majaliwa
Ugonjwa wa Macho: Walimu watakiwa kuwa waangalifu