Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Charles amekagua utekelezaji wa afua mbalimbali za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Dkt.Charles ameyasema hayo wakati alipofanya ziara Mkoani humo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Wilaya ya Kishapu.

Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu huyo amekutana viongozi na Wajumbe wa RHMT na wadau na ambapo alipata taarifa fupi ya mwenendo wa mlipuko na utekelezaji wa afua za udhibiti.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo, pia alizungumza na wataalamu na kutoa maelekezo mbalimbali muhimu ya kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa mikakati na afua hizo.

Maeneo yasiyo na migogoro yafanyiwe uwekezaji - Ulega
Hakuna nchi itakayoachwa nyuma - Majaliwa