Uongozi wa Klabu ya Young Africans umesema umeanza mchakato wa kutafuta timu za nje kwa ajili ya mechi za kirafiki itakayokiweka sawa kikosi chao katika kipindi hiki cha maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwishoni mwa juma lililopita Kocha Mkuu wa miamba hiyo ya soka nhini, Miguel Gamondi aliuomba uongozi wa timu hiyo kumtafutia mechi mbili za kirafiki na timu za nje ya Tanzania ili kujui uimara wa kikosi chake kabla ya mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na hilo pia Gamondi anataka kuitumia michezo hiyo kuwatambulisha rasmi wachezaji wao wawili wa kimataifa waliowasajili kwenye dirisha dogo la msimu huu ambao ni Augustine Okrah na Joseph Guede.

Makamu wa Rais wa Young Africans hiyo, Arafat Haji amesema wameanza kutafuta timu hizo na anaamini mchakato huo hautachukua muda kukamilika sababu wana maelewano mazuri na timu nyingi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Lengo letu ni kupata timu imara ambazo zitakipa kikosi chetu mazoezi mazuri kulingana na mashindano tunayoshiriki, ndio maana nikasema mchakato wa kuzisaka timu hizo umeanza na dhamira yetu ni kucheza mechi hizo tukiwa ugenini,” amesema Arafat.

Kiongozi huyo amesema malengo ya Young Africans msimu huu ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote, hivyo kama viongozi wa juu wanapambana kuhakikisha wanampatia kocha wao kile alichokihitaji ili kumjengea urahisi wa kufanikisha kile ambacho wamekikusudia.

Kikosi cha Young Africans kimerejea kambini Avic Town wiki mbili zilizopita kujiandaa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu na Kombe la FA huku timu hiyo ikiwakOsa baadhi ya nyota wake waliopo kwenye timu zao za taifa zinazoshiriki Afcon 2023.

Wakutana kuyapatia ufumbuzi matukio ya wizi, utapeli
RC Sendiga ataka ufanisi wa usambazaji Maji