Jeshi la Polisi Wilayani Urambo, limewahamasisha Wananchi wa Wilaya hiyo iliyopo Mkoani Tabora kujiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi, ili kudhibiti wizi wa mifugo na utapeli katika vijiji vya Kata ya Uyumbu.
Rai hiyo imetolewa na ASP Mtitu wakati akitoa elimu Wilayani humo na kuwataka Wananchi wa maeneo hayo na jirani kujenga mazoea ya kuripoti taarifa za uhalifu na wahalifu kituo cha Polisi.
Aidha, amewataka pia kutoa taarifa za Viongozi wa Vijiji au Kata ambao wanawahisi au kuwatilia shaka yakuwa wanashirikiana na wezi hasa wa mifugo ili waweze kuchukuliwa hatua.
“Vikundi vya ulinzi shirikishi (sungusungu) vinatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu na sio kuonea watu kwani vinapunguza imani kwa wananchi wenzao na kuwaona ni kama wakandamizaji na siyo watu wanaowasaidia katika ulinzi kagueni vibali vya mifugo inayopita katika vijiji inakotoka na inakoenda na kama mna mashaka mzishikilie hadi apatikane mwenye mifugo na taarifa zifike Polisi.