Mkaguzi wa Kata ya Oldeani Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Majaliwa Ernest amewaomba wazazi na walezi wa vijana wadogo kuweka ungalizi na kuwaonya baadhi ya watu wa jamii hiyo kukeketa watoto.
Ernest ameyasema hayo na kudai kuwa atahakikisha anafuatilia kwa karibu wale wote wanaofanya vitendo vya ukeketaji watoto katika kata yake ambayo kiasili ni jamii ya kifugaji na shughuli nyingine kama kilimo.
Amesema, kitendo cha kumkeketa mtoto wa kike ni kumfanyia ukatili huku akiwambia zipo sheria ambazo zitachukuliwa kwa atakaye bainika kufanya hivyo ambapo amesema zipo taarifa za baadhi ya watu wanaojihusisha kufanya hivyo akiwataka kuacha mara moja tabia hiyo.
Ameongeza kuw, jamii hiyo inatakiwa kuelewa kuwa mtoto wa kike sio mzigo bali ni dira nzuri kwa familia pale tu wazazi ama walezi watakapo jitahidi kumsomesha mtoto huyo wakike.