Mshambuliaji Mahmoud Trezeguet, anaamini uzoefu mkubwa wa Misri unaweza kuwawezesha kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’, baada ya kutinga hatua ya 16 bora kwa mbinde.

Winga huyo alipata tuzo ya nyota wa mchezo huo kwa kucheza bila kuchoka wakati Misri ilipotoka sare ya mabao 2-2 na Cape Verde na kufuzu kutoka Kundi B.

Trezeguet, ambaye alisawazisha bao la kwanza kwa Misri, amebaki na ari na morali kubwa kuhusu nafasi yao baada ya kufuzu hatua ya 16 bora.

“Kwa miaka 10 katika timu ya taifa kwangu, hakuna kitu juu ya soka,” alisema Trezeguet baada ya mechi.

“Ikimpendeza Mungu, kizazi chetu kitaondoka na kombe kwa sababu tunataka kuweka historia.”

Mchezaji huyo alisema kikosi chao kilikuwa na ari ya kupambana na ubora wa Misri unaweza kuwapeleka kwenye mafanikio.

“Tulitoa kila kitu kwa ajili ya kufuzu na wachezaji wenzetu wazuri. Sasa mashindano ya kweli yanaanza,” alibainisha Trezeguet.

Huku Misri ikiwa ndio bingwa wa kihistoria wa mashindano hayo ikitwaa mara saba, winga huyo anahisi uzoefu wa zamani unaweza kuwasaidia.

“Katika mechi za mtoano, uzoefu wetu utaleta mabadiliko, Mungu akipenda na tutafika mwisho,” alisisitiza Trezeguet kwa kujiamini.

Baada ya kusonga mbele kama washindi wa pili wa Kundi B, nyuma ya Cape Verde, Misri inaonekana kuwa na kiwango bora kwa wakati ufaao.

Akiwa na ujuzi mkubwa wa mashindano ndani ya kikosi, Trezeguet anaamini wazi kwamba ‘Mafarao’ hao wanaweza kuleta ushindi mwingine kwenye AFCON mwaka huu.

Karim Benzema kutua Arsenal, Chelsea
Max Nzengeli ana kazi maalum Young Africans