Uongozi wa Young Africans umebainisha kuwa utarejea kivingine kwenye mechi za kitaifa na kimataifa kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya ndani ya uwanja kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

Young Africans baada ya kucheza mechi 11 kwenye ligi iliambulia ushindi kwenye mechi 10 na kichapo kwenye mchezo mmoja ipo nafasi ya pili kwenye msimamo.

Kwenye michuano ya kimataifa chini ya mwavuli wa ‘CAF’, Young Africans wanashika nafasi ya pili kwenye Kundi D sawa na vinara Al Ahly wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa. CR Belouizdad wako nafasi ya tatu wakiwa na alama nne sawa na Medeama SC.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema kuwa kila kitu kinafanyika kwa mipango mikubwa na watarejea kivingine kwenye mashindano wanayoshiriki ya kitaifa na kimataifa.

“Kikubwa kwenye mechi zetu zijazo ni kufanya kazi kubwa na tunaamini kwamba tutarejea kivingine uwanjani katika kusaka ushindi ili iwe ni mwendelezo wa kufuata malengo yetu inawezekana licha ya ushindani mkubwa uliopo.

Wachezaji wanatambua kwamba kazi ni kubwa kwenye kutafuata matokeo na ushirikiano uliopo unaongeza nguvu kufanya vizuri. Bado kuna muda wa kufanyia kazi makosa yaliyopita na tunaamini tutaendelea kuwapa burudani wananchi,” amesema Kamwe.

 

Man Utd yaishtukia Inter Milan
Makala: Mkongwe Caligula na cheko la kujitekenya