Beki wa kulia wa Simba SC, Shomary Kaponbe ‘Baba Ester’ amesema bado ana misimu mitatu ya kuitumikia timu hiyo kabla ya kufikiria kustaafu.

Akizungumza beki huyo wa kutumainiwa kweye kikosi cha Kocha Abdellhak Benchikha amesema anaamini bado ana nguvu za kutosha pamoja kiwango ambacho kinamruhusu kuitumikia timu hiyo.

“Bado nina uwezo wa kuhimili ushindani wa namba katika mashindano ya ndani na nje lakini kiwango hangu bado kipo juu na sina majeraha ya mara kwa mara,” amesema Kapombe.

Mlinzi huyo alisema anatambua uongozi wa timu hiyo unasajili wachezaji wengi kutoka nje kutokana na malengo ya ushindani kwenye michuano ya kimataifa yupo tayari kupigania namba yake hadi atakapostaafu.

Amesema anachokifanya sasa ni kufanya mazoezi kwa bidii ambayo yatalinda kiwango chake na kulishawishi Benchi la Ufundi liendelee kumpa nafasi ya kucheza.

Amesena anaanini bado ana kitu cha kaifanyia Simba SC, nakuirudisha kule ilipokuwa wakati walipobeba mataji manne ya Ligi Kuu na kufika hatua ya Robo Fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kapombe ambaye kipaji chake kiliibukia akiwa timu ya vijana ya Simba SC, amekuwa mchezaji tegemeo na chaguo la kwanza la kila kocha aliyepita timu hiyo katika kipindi cha misimu sita tangu aliporejea kwa mara ya pili akitokea Azam FC.

Gamondi: AFCON 2023 itanisaidia
TUWASA punguzeni mianya upotevu wa mapato - Mahundi