Uongozi wa KMC FC umetamba na usajili wachezaji wao wapya akiwemo Shaban Chilunda kuwa utawafanya kuwa imara zaidi huku wakiweka malengo yao ya kutaka kumaliza ligi wakiwa ndani ya nne bora ili waweze kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Chilunda ni moja ya nyota wapya wa KMC ambaye amesajiliwa katika dirisha dogo akitokea Simba SC ambapo pia yupo beki, Abdalla Said Lanso kutoka visiwani Zanzibar:

Ofisa Habari wa KMC, Khalid Chukuchuku ametamba kwa kusema kuwa: “Usajili ambao KMC tumeufanya katika dirisha dogo utaona ni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu kwa ajili ya kuendelea kufanya vyema.

Tungeweza kufanya usajili hata wa wachezaji wanne au watano ambao tungewajaza bila sababu, lakini sisi tumefanya usajili wa maana na wenye tija na malengo yetu ni kuhakikisha kuwa tufanya vizuri ili tumalize ligi nafasi za nne za juu.

“Malengo yetu ni kushiriki michuano ya kimataifa na kwa usajili huu naamini utatusaidia kutimiza malengo yetu kwa ajili ya msimu ujao,” amesema kiongozi huyo.

Lookman: Umoja na mshikamano vilitusaidia
Pacome aongezewa dozi Young Africans