Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax ameipongeza JKT kwa kuendelea kuonyesha ishara ya Kujali na kudumisha upendo kwa zoezi la upandaji miti ikiwa ni Kumbukizi miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Dkt. Tax ametoa pongezi hizo hii leo Januari 29, 2023 katika zoezi la upandaji miti Lililofanyika Makao makuu ya JKT Chamwino Jijini Dodoma, ikiwa ni kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibari.
Amesema, Jeshi la Kujenga Taifa mnaonyesha ni namna gani mnajali na kudumisha upendo, najua juhudi hii ya upandaji miti ni muendelezo litakuwa na zoezi la kudumu, na najua tumejipanga kuona Makao Makuu ya Nchi yetu Dodoma inakuwa ya Kijani.”
Hata hivyo, amesema Wananchi wanapaswa kushirikiana katika kuendelea kutunza mazingira kwa kuendelea kupanda miti kila eneo ambalo linastahili, huku Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena akisema Jeshi limefanikiwa kuotesha Miti 78,800 na tunatarajia kupanda miti 100,000.
Amesema, “Jeshi la kujenga Taifa limeendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Vikosi, na katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango alitoa maelekezo kwa jeshi la JKT kutunza mazingira kwa kupanda miti ili kuendelea kuenzi muungano huo.”