Mshambuliaji  wa Nigeria, Victor Osimhen amejikuta akichaguliwa mara kadhaa kufanyiwa vipimo ili kubaini kama anatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoendelea Ivory Coast.

Hatua hiyo ya vipimo imekuwa ikifanywa na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’ kwa ajili ya ‘doping’ bila mpangilio.

Osimhen alijikuta akifanyiwa vipimo hivyo baada ya kuwa katika kiwango cha hali ya juu wakati Nigeria ilipocheza dhidi ya Cameroon na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.

CAF imekuwa ikichagua mchezaji wa kupimwa bila ya kuwa na mpangilio au utaratibu maalumu ili kubaini kama kuna mchezaji anatumia dawa hizo zilizopigwa marufuku michezoni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amedhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Nigeria waliopo katika kiwango cha juu katika mashindano haya yanayoendelea nchini Ivory Coast.

Hii ni mnara ya pili mfululizo kwa Super Eagles kucheza Robo Fainali ya ‘AFCON’.

Baada ya kuonesha kiwango bora kabisa katika mashindano hayo, nyota huyo wa SSC Napoli alijikuta akichaguliwa mara kwa mara kufanya vipimo hivyo.

Mamia ya Vijana ulinzi jamii wajisalimisha Jeshini
Mjerumani anaitaka Black Stars