Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema kuwa kazi ni moja kwa wachezaji wake kusaka ushindi kwenye mechi ambazo watakuwa wanacheza.

Timu hiyo iligotea nafasi ya pili kwenye Mapinduzi 2024, iliposhuhudia mabingwa wakiwa Mlandege wakitwaa taji hilo mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Singida Fountain Gate.

Kwenye Fainali ya Januari 13, mwaka huu iliyochezwa Uwanja wa Amaan Complex, baada ya dakika 90 ubao ulisoma MIandege 1-0 Simba SC.

Benchikha ameweka wazi kuwa wamerejea kwenye mazoezi kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi zao na wapo tayari kuendelea kuwa kwenye mwendo mzuri.

“Tumerejea kwenye mazoezi na kila kitu kinaendelea sawa. Ambacho kipo ni kuona kwamba tunakuwa kwenye kasi yetu nzuri kupata matokeo mazuri na kushinda.

Ninapenda kuona tunaendelea kushinda ndio maana tupo kwenye uwanja wa mazoezi. Wachezaji wapo wengine wapya na wengine walikuwa hapa wakati uliopita tunaendelea kufanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa.”

Katika mazoezi kocha huyo alianza kwa kutengeneza baadhi ya pacha ndani ya kkosi hicho ikiwemo ile ya ushambuliaji ambayo kwa sasa itaongozwa na Mshambuliaji Michael Fredy raia wa Ivory Coast ambaye amesajiliwa kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 16, mwaka huu.

Rui Vitoria: Ni mapema kusema hatma yangu
BMH yaandika historia tiba ya Selimundu