Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera, Christopha Parangyo amelazimika kumpigia Simu Meneja wa Tarura Mkoa wa Kagera, Mhandisi Avith Teodory ili kupata ufafanuzi wa ubovu wa Barabara ya kafunjo Rubale yenye urefu wa kilometa 18 iliyo kikwazo cha mawasiliano kwa Wananchi wa Kata ya Rubale.

Akizungumza wakati wa mkutano wake na Wananchi wa Kata hiyo Wilaya Bukoba kwenye maadhimisho ya Chama cha Mapinduzi CCM kupitia UWT Mkoa Kagera, amesema wananchi wamekuwa wakipata adha wakati wa kutumia Barabara hiyo.

Akijibu kero hiyo, Mhandisi Avith Theodory amewaondoa hofu wananchi hao akisema Barabara hizo zimeathiriwa na mvua ambazo zilikuwa zikinyesha na tayari wamesha anza jitihada kumpata mkandarasi wa kufanya matengenezo.

BMH yaandika historia tiba ya Selimundu
Hersi Said: Tutamuuza Stephane Aziz Ki