Wanawake wa UWT Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, wameadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kupanda miti ya vivuli na Matunda 107 na kufanya usafi katika Shule ya Sekondari ya Ridhiwani Kikwete, iliyopo katika Kata ya Kiwangwa.
Akizungumza wakati wa upandaji miti huo Mwenyekiti wa UWT, Mariamu Mkali amesema maadhimisho hayo yafanyika kwenye Kata hiyo na UWT Wilaya ya Bagamoyo wamechagua kupanda miti kwa kuwashirikisha Madiwani Viti maalumu, Viongozi na Wanafunzi wa Shule hiyo.
Aidha, aliwakata Wanafunzi wa Shule hiyo kusoma kwa bidii kwa kuthamini mchango wa Wazazi wao wanaosomesha kwa kumtanguliza Mungu katika masomo yao, ili awalinde na vikwazo na changamoto mbalimbali na wafikie malengo yao ya maisha.
Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Bagamoyo Catherine Makungwa alisema pia walitembelea na kukagua Maendeleo ya Zahanati ya Kata ya Kiwangwa na kushiriki ujenzi wa Moja ya madarasa ya shule hiyo na kufanya mkutano wa ndani wa hadhara, uliohusisha wanaCCM na Wananchi kwa ujumla.