Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamisi Juma amesema uhalifu unaoendelea kufanyika Nchini ni pamoja na utakatishaji fedha, ufadhili wa kigaidi na matumizi ya silaha zisizo halali.
Kauli hiyo, ameitoa mbele ya Majaji wa Mahakama za Rufani, Mahakama kuu ya Tanzania, Wananchi na Wadau wengine wa sekta ya sheria, walioshiriki kongamano la siku moja la kujadili masuala ya makosa ya uhalifu wa kifedha jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto – IJA, na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dkt. Paul kihwelo akizungumzia suala hilo amesema wapo kwenye mkakati wa kukabiliana na mbinu zinazotumiwa na wahalifu, ili kupunguza hali hiyo.
Kupitia kongamano hilo, mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania utatoa nafasi kushirikiana na wadau kutafuta changamoto zinazoikumba sekta ya sheria na utoaji haki.