Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari kuongeza jitihada, ili kuinua zaidi kiwango cha ufaulu.
Makongoro ameyasema hayo wakati wa kikao cha tathmini tathmini ya shughuli za elimu Mkoani Rukwa kwa Mwaka 2023, kilichofanyika mjini Sumbawanga.
Amesema, Viongozi wote kuanzia ngazi za mitaa hadi Mkoa kwa kushirikiana na Walimu na Wazazi wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula chenye lishe bora mashuleni, ili kusaidia kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Rukwa pia amewataka Viongozi wote, Wazazi na Walimu kukomesha utoro kwa Wanafunzi, kwani unachangia kwa kiasi kikubwa, Wanafunzi kufeli.
Hata hivyo, Makongoro pia amewapongeza Walimu na Wadau wote wa Elimu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuinua kiwango cha taaluma, Mkoani Rukwa.