Winga wa Timu ya Taifa ya Senegal ‘Simba wa Teranga’, Krepin Diatta huenda akakumbana na adhabu kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ baada ya kulituhumu kula rushwa kufuatia mabingwa hao watetezi wa Afrika kutupwa nje kwa mikwaju ya Penati mbele ya Ivory Coast kwenye mchezo wa Hatua ya 16 Bora katika Fainali za AFCON 2023, Jumatatu (Januari 29).

“Mmetuua. Mmekula rushwa. Kaeni na kombe lenu,” alisema winga Diatta, anayekipiga kwenye klabu ya AS Monaco alipokuwa akiwashambulia viongozi wa CAF mjini Yamoussoukro.

Ivory Coast ilishinda kwa Penati 5-4 baada ya sare ya bao 1-1, huku Senegal wakiendeleza Rekodi ya kumshuhudia Bingwa Mtetezi akishindwa kutetea taji la AFCON 2023, ambapo hakuna timu nyingine iliyowahi kufanya hivyo tangu Misri iliponasa taji kwa mara tatu mfululizo mwaka 2010.

Diatta alikasirika kwa sababu Senegal haikupewa Penati kipindi cha pili wakati Ismaila Sarr alipoangushwa ndani ya boksi kwa kubanwa miguu na beki wa Ivory Coast, Odilon Kossounou.

Senegal iliongoza 1-0 kwa bao la mapema la Habib Diallo, lakini mwamuzi wa Gabon, Pierre Ghislain Atcho hakuamuru Penati wala kwenda kwenye VAR kutazama marudio aliyochezewa Sarr ndani ya boksi la Ivory Coast, ambao ni wenyeji wa Fainali hizo za ‘AFCON 2023’.

 

 

GGML kinara ukuzaji mahusiano sekta ya Madini - Dkt. Mwigulu
Walioiba Majeneza Msikitini kusomewa kisomo