Walimu Wakuu katika shule za Serikali Nchini Kenya, wametakiwa kuchapisha kiwango cha karo wanachowatoza Wazazi na kuwasilisha ripoti hiyo katika Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kabla ya Februari 10, 2024.
Kupitia taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari, Katibu wa Wizara ya Elimu, Belio Kipsang pia amewaagiza wasimamizi wa elimu nyanjani, kufuatilia na kuhakikisha kuwa shule zote zinazingatia sheria ya ulipaji karo iliyotolewa na Wizara hiyo.
Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa wale wote watakaoenenda kinyume na agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi.