Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amelitaka Jeshi la Polisi Idara ya Upelezi kuongeza bidii na kasi katika kupeleleza kesi za jinai ili Mahakama iweze kutoa haki kwa wakati.

Serukamba aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Sheria Mkoa wa Singida na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza watendaji wa Mahakama na wadau wake kwa kazi nzuri wanayofanya japo changamoto zipo.

Awali, Hakimu Mfawidhi wa .ahamaka Mkoani Singida, A Nzowa alisema wadau wa Mahakama ambazo ni taasisi za haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi, TAKUKURU, Mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kitengo cha kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya, wana nafasi muhimu katika mnyororo wa utoaji haki.

Ameliomba Jeshi la Polisi na taasisi zingine za uchunguzi kuanzisha mfumo jumuishi wa TEHAMA utakaosaidia kufuatilia mwenendo wa vielelezo kutoka taasisi moja kwenda taasisi nyingine ili kurahisisha utoaji haki kwa wakati.

Mjadala ununuzi Dawa adimu toka Cuba wafanyika
Wahimizwa matendo mema kujenga kizazi adilifu