Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouf Dabo amewaomba Washambuliaji wake kufunga mabao ya kutosha kwani yatawasaidia katika harakati zao za kusaka ubingwa msimu huu.

Akizungumza kocha huyo amesema mpaka sasa timu yake ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, huku wakifunga mabao mengi jambo ambalo wanapaswa kulitilia mkazo.

“Tumeshuka hadi katika nafasi ya pili baada ya wapinzani wetu Young Africans kushinda mchezo wao wa jana dhidi ya Dodoma jiji, nimewaambia washambuliaji waongeze umakini na kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza katika kila mchezo,” amesema Dabo.

Kocha huyo kutoka nchini Senegal amesema anafurahishwa na idadi ya mabao ambayo wameyafunga kwenye mechi zilizopita lakini amewataka washambuliaji wake waongeze umakini ili kufunga mabao mengi zaidi ya hayo.

Amesema katika ligi yenye ushindani kama hii bingwa kupatikana kwa wingi wa mabao si ajabu ndio maana amekuwa akipambana sana na safu yake ya ushambuliaji kwa kuwa ndiyo iliyoshikilia hatima ya malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Katika michezo 13 iliyocheza ya mzunguko wa kwanza Azam FC imefunga mabao 35 na kuruhusu mabao 10 wakati wapinzani wao Young Africans waliopo kileleni, wamefunga mabao 31 na kuruhusu mabao sita.

Chama: Tusahau yaliyopita, nitapambana
Mashine mpya Man City 2024/25