Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, mastaa wa Young Africans wametamba kuwa sasa hawashuki tena kileleni mpaka watakaposhinda ubingwa.

Young Africans juzi Jumatatu (Februari 05) walikuwa wenyeji wa Dodoma katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kuwashuhudia wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 amnbalo lilifungwa na Mudathir Yahya.

Ushindi huo uliifanya Young Africans kufikisha pointi 34 na kujichimbia kileleni mwa msimamo wakifuatiwa na Azam FC ambao wanakamata nafasi ya pili na pointi zao 31, huku watani za wa jadi Simba SC wakiwa nafasi ta tatu kwa kuwa na point 29.

Mfungaji wa bao pekee la Young Africans kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Mudathir amesema ushindi huo umezidi kuwaongezea ari ya kutetea ubingwa wao kwa mara ya tatu mfululizo.

“Tumefurahi kupata ushindi huu ambao naweza kusema ulikuwa muhimu kutokana na matokeo ambayo tuliyapata mkoani Kagera. Ni wazi ulikuwa mchezo mgumu na wapinzani wetu walionyesha upinzani mkubwa.

“Ushindi dhidi ya Dodoma Jiji umeongeza ari yetu kama kikosi katika kuhakikisha tunaongeza nguvu kupambana na kushinda michezo yetu iliyosalia ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa tena msimu huu.”

RC fuatilia bei ya Sukari chukua hatua - CDE Kawaida
Uwanja Azteca kufungua Kombe la Dunia 2026