Jopo la watu tisa litaamua washindi wa vipengele tofauti katika Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoelekea ukingoni nchini Ivory Coast vikihusu wachezaji, makocha na tỉmu za taifa zilizoshiriki.

Vipengele hivyo vinahusu tuzo za mchezaji bora wa mechi, mchezaji bora wa mashindano, mchezaji bora chipukizi, kipa bora, kocha bora na timu yenye nidhamu.

Mkurugenzi maendeleo ya ufundi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, Rau Chipenda ndiye anaongoza jopo hilo lililosheheni nyota wa zamani wa soka wa mataifa tofauti ya Afrika ambao walitengeneza majina yao kipindi wanacheza soka.

Kipa wa zamnani wa Cameroon, Joseph Antoine Bell ni miongoni mwa wajumbe wa jopo hilo akiwepo pia kocha na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco, Jamal Fathi pamoja na mtaalamu wa ufanisi, Abdul Faisal Chibsah kutoka Ghana.

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda ambaye kwa sasa ni Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini humo (FUFA), Edgar Watson pia anaunda jopo hilo ambalo pia linawajumuisha Clementine Toure (Ivory Coast), Herita Ilunga (DR Congo), Abraham Mebratu (Ethiopia) na Michael Amenga wa Kenya.

Mbali na washindi wa vipengele tofauti mashindano kuteua hayo, jopo hilo pia lina jukumu la kuandaa ripoti ya kiufundi ya mashindano hayo ambayo fainali yake itachezwa Februari 11 jijini Abdjan, Ivory Coast.

Jurrien Timber arudushwa kundini
Msiwafunge Biashara, wapeni elimu ya kodi - Meya Kagera