Wakati wenyeji Ivory Coast na Nigeria zikitarajiwa kucheza Fainali Jumapili (Februari 11) katika michuano ya Kombe Mataifa Afrika ‘AFCON 2023’, mchezaji wa zamani wa ‘Super Eagles’, Daniel Amokachi, amelipongeza Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, kutokana na mwenendo mzuri wa michuano hiyo msimu huu.

Amokachi amekaririwa akisema kuwa CAF imejipanga vyema kuendesha na kufanikisha fainali za mwaka huu ambazo hazina dosari.

Amesema tangu alipowasili nchini Ivory Coast, ameona mabadiliko makubwa ukiwemo mpangilio wa ratiba za mashindano, maeneo yote vilipo viwanja vinavyotumika.

Viwanja vinavyotumika vimejengwa kwa ustadi mkubwa na vya kisasa, huduma zote muhimu zinapatikana kwa wakati, ninaipongeza CAF kwa kufanya maandalizi mazuri na kuifanya michuano ya msimu huu kuwa kivutio,” amesema Amokachi.

Nyota huyo wa zamani aliwahi kuingoza Nigeria kutwaa taji la AFCON akiwa mchezaji mwaka 1994 kisha akiwa akiwa Kocha Msaidizi chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, marehemu Stephan Keshi mwaka 2013, nchini Afrika Kusini.

Vyanzo vya Umeme kuanzishwa kukidhi mahitaji - Dkt. Biteko
Bei ya mwamba imefichwa Old Trafford