Takriban Polisi sita wamejeruhiwa huku watu 13 wakiwekwa kizuizini, baada ya kutokea kwa vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa serikali ya Eritrea kwenye mji wa The Hague, nchini Uholanzi.
Vurugu hizo pia zimesababisha uharibifu wa mali, huku Polisi wakisema maafisa wake na wahudumu wa huduma ya dharura walipigwa mawe na fataki wakati makundi hayo mawili yanayopingana yalipoanza mapambano.
Aidha, Magari mawili ya Polisi na basi moja yaliteketezwa, huku magari mengine yakiharibiwa vibaya katika eneo la eneo la mkutano lililoandaliwa na kundi linaloiunga mkono serikaya Eritrea.
Hata hivyo, Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kutuliza ghasia, huku Meya wa mji wa The Hague, Jan van Zanen akilaani ghasia hizo na kutangaza hali ya hatari katika eneo la tukio.