Mtu mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha gari la abiria aina ya Tata lenye namba za usajili T 596 EAF kugongana uso kwa uso na Bajaji.
Ajali hiyo, imetokea eneo la Mindu lililopo Barabara kuu ya Morogoro kuelekea Iringa, huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa basi la abiria kuhama upande wake bila kuchukua tahadhari.
Daktari wa Kitengo cha dharula Hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro, Joseph Kwai amethibitisha kupokea mwili wa marehemu ambaye ni Mwanamke aliyekuwa abiria wa bajaji na majeruhi wa basi na bajaji.