Rais Samia Suluhu Hassan atafungua Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ‘CISM’, utakaofanyika kuanzia Mei 12 hadi 19 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Wakili Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, Meja Jeneral, Francis Mbindi amesema mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa mzunguko na mwaka jana ulifanyika Ulaya katika nchi ya Russia.

Amesema mkutano huo utakuwa wa siku saba utakaoanza Mei 12 hadi 17 mwaka huu na utahudhuriwa na wanachama wote nchi 140 duniani.

“Na kwa kuzingatia mkutano huu ni wa kijeshi na washiriki ni wanajeshi kutoka nchi zote duniani huwa tuna desturi ya kutembelea maeneo ambayo yametoa mchango wa kuleta uhuru katika nchi ambazo mkutano unafanyika,” amesema.

Amesema kwa upande wa Tanzania washiriki watatembelea mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa Mnazi Mmoja jjini Dar es salaam na kwamba watatoa heshima kwa Mashujaa walioshiriki katika kuiletea uhuru nchi na kuweka mashada ya maua.

Meja Jenerali Mbindi amesema faida nyingine kutoa fursa ya kutangazwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu itakuvwa ni miongoni mwa lugha tano zitakazotumika katika mkutano huo.

AMEsema watakuwa na programu katika mkutano huo itakayojulikana kama siku ya utalii, ambapo washiriki wote watapelekwa katika vivutio vya utalii vilivyopo Dar es salaam.

Baraza la michezo ya majeshi duniani liliundwa februari 18 mwaka 1945 baada ya vita kuu ya pili vya dunia na hadi sasa lina nchi wanachama 140.

Kampuni binafsi zitumie mwogozo wa GGML kuibua vipaji - TPSF
Freddy Koublan: Ninawafahamu vizuri Asec