Afarah Suleiman, Magugu – Manyara.

Kufuatia tukio la ufungaji njia na uwepo wa maandamano ya Wananchi katika mji wa Magugu uliopo Wilayani Babati Mkoani Manyara, wakishinikiza kutolewa kwa mtu mmoja ambaye anashukiwa kwa tuhuma za mauwaji ya mtoto (7), Jeshi la Polisi limesema limefanikiwa kutuliza ghasia hizo na sasa hali ni shwari.

Kwa mujiwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP George KatabaziĀ  amesema wamefanikiwa kumaliza vurugu hizo bila kuathiri mali za Wananchi au kusababisha kifo.

Amesema Jeshi la Polisi lipo imara na wamemshikirika mtu huyo kwa mahojiano na pindi uchunguzi utakapo kamiliaka utaratibu wa sheria juu yake utafuata.

Aidha Kamanda Katabazi amewataka wananchi kuwa watulivu na kuacha kujichukulia Sheria mkononi,mpaka hapo uchunguzi utakapo kamilika na Mtuhumiwa kufikishwa mahakani.

Watendaji wa CCM waula Bima ya Afya Msoga
Polisi wafanikiwa kudhibiti wizi kupitia Bodaboda Moro