Scolastica Msewa, Msoga – Pwani.

Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekabidhi kadi za Bima ya afya 180 kwa Mabalozi wa Nyumba kumi, wenyeviti wa CCM Tawi, Makatibu wa CCM Tawi na Makatibu Uenezi wa Matawi ya CCM wa Kata ya Msoga jimbo la Chalinze mkoani Pwani, ili kuwarahisishia namna ya kupata huduma za afya.

Ridhiwani amekabidhi kadi hizo wakati Diwani wa Kata ya Msoga, Hassan Mwinyikondo akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili ya 2012/2022 na 2022/2023, katika Viwanja vya ofisi ya Kata ya Msoga, hafla iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CCM ngazi ya Kata na Wilaya na Serikali.

Amesema, lengo la kugawa kadi hizo ni kulinda na kuthamini mchango wao mkubwa kwa CCM ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa Mabalozi hao wa Nyumba kumi, Makatibu wa CCM na Makatibu wa uenezi wa CCM Tawi, ili wawe na afya njema kila siku pasipo kutetereka kiafya .

Amesema, kwa pamoja wanatakiwa kushikamana hasa katika kipi di hiki ambacho kwachama kinaelekea katika chaguzi za serikali za mitaa ili kuweza kupata ushindi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani kata ya Msoga Hassani Mwinyi kondo amesema CCM inawapenda na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Mabalozi hao wa Nyumba kumi, makatibu wa CCM tawi na Makatibu wa uenezi wa CCM tawi ndio maana wametoa kadi hizo za afya kwao.

Amesema kata ya Msoga imetekeleza Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4 na Milioni mia sita Katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na wanampango wa kujenga Zahanati Katika kijiji Cha Msoga kutokana kilichokuwepo kupandishwa hadhi Hadi kufikia hospitali ya Wilaya.

Naye Diwani Viti maalumu tarafa ya Msoga, Debora Rashidi amemshukuru Rais Dkt. Samia kwaajili ya kukamilika kwa wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya Msoga ambapo Sasa pia huduma ya upasuaji wa mabusha na matende unafanyika hospitalini hapo.

Amesema, huduma ya upasuaji wa mabusha na matende wilayani Bagamoyo ni huduma muhimu kwani kuna akinababa wanasumbuliwa na mabusha na matende wilayani humo hivyo wanahitaji kufanyiwa upasuaji ambapo Sasa huduma hiyo inatolewa hospitalini hapo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 22, 2024
Polisi wafanikiwa kudhibiti vurugu bila uharibifu Babati