Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wanadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 100 Milioni katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kumuuza kiungo Kevin De Bruyne ambapo timu mbalimbali kutoka Saudi Arabia zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa De Bruyne kuhusishwa na Saudia mara ya mwisho ikiwa ni misimu kadhaa iliyopita lakini Man City inadaiwa kwamba ilikataa kumuuza.
Staa huyu ambaye mkataba wake unamalizika 2025 hadi sasa hajasaini mkataba wa kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho.
Moja ya sababu zinazodaiwa kuifanya Man City iwe tayari kumuuza ni rekodi ya majeraha ya mara kwa mara inayomuandama jambo linalosababisha awe nje ya Uwanja kwa muda mrefu.
Ikiwa atatua Saudia atakuwa ni mchezaji wa tatu kutoka Man City kwenda kukipiga baada ya Riyah Mahrez anayeichezea Al Ahli na Aymeric Laporte wa Al Nassr.