Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Beyern Munich wanaamini Alphonso Davies ana uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa majira ya joto kuliko kusaini mkataba mpya Allianz Arena, kwa mujibu wa ripoti.
Mkataba wa Davies hapo Bavaria utaendelea hadi mwaka 2025 na mazungumzo hayajaendelea juu ya makubaliano mapya, na hivyo kuongeza uwezekano wa kuondoka wakati wa majira ya joto.
Real Madrid wamekuwa wakijaribu kumshawishi Davies msimu mzima na inasemekana wanamwona kama mmoja wa walengwa wao wa uhamisho pamoja na Kylian Mbappe wa PSG.
Sky Sports Ujerumani imeripoti kuwa Madrid haitakuwa na tatizo kukubaliana na Davies na wanatarajiwa kuwapa Bayern ada ya juu.
Lakini Los Blancos’ wanaweza kujaribu kupunguza idadi hiyo ikiwa mkwamo wa mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada utaendelea hadi msimu wa majira ya joto.
Mkurugenzi wa wa Michezo wa Bayern, Christoph Freund, hivi karibuni alikuta- na na wakala wa Davies mjini zaidi ya euro milioni 50.
Munich, na hisia kutoka kwa mabingwa hao wa Ujerumani ni kwamba beki huyo wa kushoto ana uwezekano mkubwa wa kuuzwa katika dirisha la majira ya joto.
Beki ya kushoto imekuwa tatizo pale Madrid hadi msimu huu, huku Ferland Mendy akizunguka ndani na nje ya timu kutokana na jeraha na usajili wa majira ya joto wa Fran Garcia ambaye ameshindwa kutumia vema mechi zake chache hadi sasa.
Kiungo Eduardo Camavinga amelazimika kujaza nafasi ya beki wa kushoto katilka mechi mbalimbali kwa mwaka mzima.