Hafla ya utiaji saini Mkataba wa Upembuzi yakinifu kwa ajili ya ununuzi wa Meli za uvuvi katika Bahari kuu na ujenzi wa Viwanda viwili vya kuchakata Samaki, kitakachojengwa Kilwa Kivinje Bara na kingine Fungurefu, Zanzibar imekamilika hii leo Februari 27, 2024.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jimmy Yonanzi amezipongeza kampuni za DMG na TANSHEQ ambazo zimeingia ubia na kushinda zabuni hiyo.

Amesema, “ni vyema mkafahamu kuwa, Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ni moja ya Programu za kitaifa za kimkakati zilizo katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.”

Aidha Dkt.Yonaz ameongeza kuwa, “na lengo ni kuimarisha uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja na Taifa, pamoja na kuendeleza uchumi wa buluu. Hivyo, mkifanya kazi hii kwa weledi na kukamilisha kwa wakati uliopangwa mtakuwa mmeshiriki katika kutafsiri maono ya Viongozi wetu wakuu ”

Hata hivyo, amewasihi wakati wa utekelezaji wa zoezi hili la Upembuzi Yakinifu, na watakapopata changamoto yoyote, Wasisite kuwasiliana na ofisi kwa utatuzi wa haraka.

“Ninawasihi kuwa, wakati wa utekelezaji wa zoezi hili la Upembuzi Yakinifu, mara mtakapopata changamoto yoyote, tafadhali msisite kuwasiliana na ofisi yangu kwa utatuzi wa haraka ili tuweze kukamilisha zoezi ndani ya muda tuliokubaliana”, aliongeza Dkt. Yonaz.

Anthony Martial kuondoka Man Utd
Kidunda: Asemahle Wellem hatanisahau