Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Kamanda wa Polisi Mkoa Manyara, SACP George Katabazi ameshiriki ujenzi wa kivuko cha muda ambacho alihadi kukijenga katika Kijiji cha Mapea kilichopo Kata ya Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Ahadi hiyo aliitoa katika Mkutano na Wananchi wa Kijiji hicho, kufuatia kifo cha mtoto (7), ambaye aliuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwili wili katika eneo hilo la shamba la mwekezaji Odedra Odedra februari 20, 2024.

Akiwa katika eneo hilo la kivuko, Katabazi amesema wameamua kujenga kivuko hicho cha muda, ili Wananchi waweze kupita kwa urahisi ikiwa ni pamoja na magari ya Polisi kuweza kufanya doria na kukomesha vitendo vya kihalifu.

Kufuatia ujenzi huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapea, Philemon Mbogo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwasaidia magogo kwa aji ya kujenga kivuko hicho cha muda na kuahidi kukitunza.

Aidha, kwa upande wao Wananchi wa Kijiji hicho wameshukiru kwa kivuko hicho wakidai walikuwa wakipata shida katika eneo hilo lililokuwa na matukio ya kikatili na kihalifu mara kwa mara.

Pep Guardiola amuonya Jack Grealish
Uwanja wa Soka Arusha kuanza kujengwa