Majogoo wa jiji ‘Liverpool’ hawana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kumpoteza mlengwa wao mkuu wa ukocha, Xabi Alonso kwenda Bayern Munich, kwani klabu hizo zinasaka kocha mpya huku mabosi wao kwa sasa wakitarajiwa kujiuzulu mwishoni mwa msimu huu.
Jurgen Klopp alithibitisha kuondoka kwake Anfield Januari baada ya kufanya uamuzi kwa faragha mwezi Novemba, huku Thomas Tuchel akiondoka Allianz Arena majira ya joto.
Inaelezwa kuwa anayeongoza orodha ya makocha saba wanaowaniwa na Liverpool kuchukua nafasi ya Klopp ni Alonso, ambaye yuko mbioni kuiongoza Bayer Leverkusen kutwaa taji lao la kwanza kabisa la Bundesliga msimu huu.
Lakini Bayern sasa pia wako sokoni kutafuta kocha na Alonso ndiye mgombea mkuu kuchukua mikoba ya pale Bavaria.
Licha ya hayo, vyanzo vinaeleza kwamba Liverpool hawajashtushwa na maslahi haya ya wapinzani na wanaamini kuwa wanadhibiti hali hiyo.
Hisia za Liverpool ni kama hawatamchukua Alonso, itakuwa ni kwa sababu wana mgombea mwingine akilini mwao kwa kazi hiyo, badala yake wekundu hao wanatarajia kuteua Mkurugenzi mpya wa michezo katikati ya mwezi Machi kabla ya kukamilisha kuajiri kocha.
Inachukuliwa kuwa muhimu Mkurugenzi wa michezo kuja kwanza, na labda hata aina tofauti ya muundo na safu ya majukumu mapya ya kuajiri na vyeo.