Kiungo wa kati wa Real Madrid, Toni Kroos amesema “sikuwahi kutilia shaka uamuzi wangu” kurudi kucheza soka la kimataifa ili kuiwakilisha Ujerumani kwenye michuano ya Euro 2024.

Kroos aliachana na majukumu ya kimataifa karibu miaka mitatu iliyopita baada ya michuano ya Euro 2020 iliyokatisha tamaa.

Ujerumani tayari ilikuwa na wakati mbaya kwenye Kombe la Dunia 2018 iliposhindwa kutoka katika hatua ya makundi, kisha ikarudia makossa hayo mwaka 2022 bila Kroos.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alithibitisha wiki iliyopita kuwa atarejea katika kikosi cha Ujerumani mwezi ujao.

Akienda kwa undani zaidi kuhusu uamuzi huo, Kroos alieleza kwenye podikasti yake ya Einfach mal Luppen: “Hakujawa na wakati ambapo nilitilia shaka. Pengine isingekuwa vyema kusema hivyo sasa, lakini ni kweli kutoka chini kabisa ya moyo wangu.

“Ningesema kwamba nilifikiria kila kitu vizuri. Nilichukua muda wa kutosha kufikiria kila kitu na nikafikia hitimisho kwamba nafasi bado ninayo.”

Ujerumani itakuwa kwenye ardhi ya nyumbani msimu wa joto, wakitaka kushinda taji la kwanza la kimataifa tangu Kombe la Dunia mwaka 2014. Mafanikio yao ya mwisho ya Ubingwa wa Ulaya yalikuja mwaka 1996.

Kuhusu mustakabali wa klabu yake, Kroos ana mkataba na Real Madrid hadi Juni.

Hakusaini mkataba huo hadi mkataba wake wa awali ukiwa umesalia siku chache kumalizika msimu uliopita wa joto na anaweza tena kuchelewesha uamuzi wowote kuhusu msimu ujao hadi mwishoni mwa msimu, au hata baada ya mkataba wake kumalizika.

Joan Laporta ambembeleza Xavi
Liverpool kumpotezea Xabi Alonso