Kiungo Mshambuliaji wa Chelsea, Raheem Sterling haonekani kupendezwa na tetesi za uhamisho wa kwenda Ligi Kuu ya Saudi Arabia, huku mabingwa Al Hilal wakionesha nia ya kumtaka.
Watu wengi wenye majina makubwa Barani Ulaya bado wanahusishwa na uhamisho wa kwenda kwenye taifa hilo tajiri la Ghuba, lililochochewa na mabadiliko ya Cristiano Ronaldo kwenda AI Nassr mwishoni mwa 2022.
Lakini Sterling anaonekana kusita, kwani mwandishi nguli wa michezo, Fabrizio Romano ameripoti kwamba kambi yake haijawahi kushiriki au kujadili uwezekano wa uhamisho wa kwenda AI Hilal.
Fabrizio pia aliwanukuu wawakilishi wakisema: “Raheem amejitolea kama zamani katika mradi wa Chelsea.”
Baada ya kukaa kwa miaka 12 kaskazini magharibi mwa England akiwa na Liverpool na Manchester City, nyota huyo wa zamani wa akademi ya QPR, Sterling alirejea London mwaka 2022 kujiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 50.
Alikuwa ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu England akiwa na City, na hata alifunga mabao 31 katika mashindano yote msimu wa 20O19/20 pekee.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hajawa katika kiwango bora akiwa na kikosi cha Chelsea katika kipindi cha hivi karibuni kutokana na mabadiliko makubwa ya wachezaji.
Sterling ameanza mechi nyingi za Ligi Kuu kwa Chelsea msimu huu, lakini amefunga mara moja pekee kwenye mashindano yote tangu mwishoni mwa Novemba, licha ya bao muhimu katika sare ya 1-1 dhidi ya klabu yake ya zamani.
Kushuka kwa kiwango na kuongezeka kwa umuhimu wa wachezaji kama Bukayo Saka na Phil Foden pia kumesababisha nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kuwa hatarini, na hajaitwa tangu Kombe la Dunia la 2022.
Licha ya Sterling kutokuwa na mpamgo huo, lakini klabu za Ligi Kuu Saudia hazitapunguza matarajio yao wakati dirisha la usajili la majira ya joto linapokaribia.