Taifa la Somalia, limejiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwa taifa la nane mwanachama wa taasisi hiyo ya kikanda ambapo Bendera yake ilipandishwa rasmi kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha, hii leo Mchi 4, 2024.
Hatua hiyo, inafuatia Somalia kuwasilisha hati yake ya kuridhia kujiunga na Jumuiya hiyo kongwe zaidi barani Afrika ambapo Waziri wa Biashara na Viwanda wa Somalia, Jibril Abdirashid Haji Abdi ndiye aliwasilisha hati ya kuridhia taifa hilo kuwa mwanachama rasmi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hati hiyo, iliyokabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Peter Mathuki akisema, “Hatua hii itaiwezesha Somalia kuchangia katika utekelezaji wa mipano mbali mbali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Umoja wa Forodha, Soko la pamoja, Umoja wa Fedha na Shirikisho la kisiasa,”
Hata hivyo, amebainisha kuwa Somalia itanufaika na miradi ya miundombinu ya kikanda kama vile barabara, reli na nishati.