Baada ya kupita kwenye hatua ya makundi, sasa Simba SC na Young Africans zitajua zitakutana na nani kwenye hatua ya Robo Fainali katika droo ambayo itachezeshwa Machi 12, 2024 huko Cairo, Misri.
Simba SC na Young Africans ambazo zote zimefuzu kwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao zitakuwa macho kutazama wapinzano wao hao kuanzia saa l0:00 jioni ambapo Droo hiyo ndio itaanza.
Young Africans iliyomaliza Kundi D, kwa alama nane inatarajiwa kukutana na timu moja kati ya tatu ambazo zimemaliza nafasi ya kwanza kwenye makundi mengine ambapo kuna Asec Memosas, Mamelodi Sundown na Petro Atletico de Luanda.
Kwa upande wa Simba SC ambayo ilimaliza ya pili katika kundi B ikiwa na alama tisa, itakutana na timu mojawapo kati ya Mamelodi, Al Ahly na Petro de Luanda.
Mbali ya Droo hiyo ya Ligi ya Mabingwa pia kutakuwa na Droo ya Kombe la shirikisho hapo hapo jijini Cairo itakayotangulia kuchezeshwa kuanzia saa 9:00 alasiri.
Timu nane zilizofuzu Robo Fainali kwenye Ligi ya Mabingwa ni pamoja na mabingwa mara 11 ambao pia ni watetezi wa taji hilo Al Ahly ya Misri, ASEC Mimosas (Ivory Coast), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Petro de Luanda (Angola), TP Mazèmbe (DR Congo), Simba SC (Tanzania), Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) na Young Africans ya Tanzania.
Kwa upande wa Kombe la Shirikisho timu za Robo fainali ni USM Alger (Algeria), Zamalek (Misri), Dreams FC (Ghana), RS Berkane (Morocco), Modern Future (Misri), USM Alger (Algeria), Zamalek (Misri), Dreams FC (Ghana), RS Berkane (Morocco), Modern Future (Misri), Abu Salem (Libya), Rivers United (Nigeria), Stade Malien (Mali), Abu Salem (Libya), Rivers United (Nigeria), Stade Malien ya Mali.