Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umesema umejipanga kikamilifu kuhakikisha timu yao inapata ushindi katika mechi nne za Ligi Kuu Tanzania Bara wanazotarajia kucheza kuanzia kesho Ijumaa (Machi 08).

Kikosi cha Young Africans kimeanza safari mapema leo Alhamis (Machi 07) kuelekea Ruagwa mkoani Lindi tayari kwa mchezo huo wa Ligi Kuu.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema sababu ya kuzipa uzito mechi hizo ni kutokana na kubeba matumaini ya kutetea taji hilo ambalo wanalishikilia kwa misimu miwili mfululizo.

“Tuna mechi nne za ligi kabla hatujarudi kwenye mchezowetu wa Robo Fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho tutacheza na Namungo na baada ya hapo tutacheza na Ihefu baadae Azam FC, tumejpanga kuhakikisha mechi zote hizi tunapata ushindi sababu pamoja na kuongoza, lakini pointi tulizonazo bado hazijatosha kutufanya kuwa mabingwa wa ligi msimu huu,” amesema Kamwe.

“Tunatambua kwamba mechi hizo zipo karibu ambapo timu itakuwa inapumzika siku mbili kabla ya mchezo nwingine, lakini kwa upana wa kikosi tulichonacho chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi uwezokano wa kutimiza lengo upo kwa kiasi kikubwa.”

Akiuzungumzia mchezo dhidi ya Namungo, Kamwe amesema anajua utakuwa mgumu kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza ambao walishinda bao 1-0, lakini kuimarika kwa kikosi chao na utayari waliokuwa nao unawapa matumaini ya kubeba alama zote tatu katika mchezo huo.

Wakati huo huo, Kamwe amesema kwa ubora wa kikosi chao wapo tayari kupangwa na timu yoyote katika hatua ya Robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Droo ambayo inatarajiwa kuchezeshwa Machi 12, mwaka huu nchini Misri.

“Ingekuwa timu inaruhusiwa kuchagua wa kucheza naye basi yuko mtu ambaye tunamtamani ili tumalize utata, lakini kwa kuwa mpinzani anajulikana kwa kuchezeshwa Droo tunasubiri kumjua lakini tupo tayari kupangwa na timu yoyote kati ya Mamelodi Sandowns, Petro Atletico na Asec Mimosas,” amesema

Mjadala wa Prince Dube umefungwa rasmi
Bayern Munich kuizidi kete Liverpool