Gwiji wa FC Barcelona, Gerard Pique, amewaonya viongozi klabu hiyo kuacha kuwahadaa mashabiki wao na kuihimiza klabu hiyo kuwa wazi kuhusu hali yao.
Barca ina takriban euro milioni 200 zaidi ya kikomo cha matumizi ya kila mwaka cha euro milioni 204 kilichowekwa na La Liga, jambo ambalo linawazuia kusajili wachezaji wapya wanaoweza kusajiliwa au kuongeza mikataba mipya.
Uwanjani wameachwa kwa pointi nane nyuma ya vinara wa La Liga Real Madrid na kutupwa nje ya Copa del Rey na Spanish Super Cup tangu mwanzoni mwa mwaka.
Wamebakia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku mechi yao ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora dhidi ya SSC Napoli ikichezwa wiki ijayo, lakini Pique hajashawishika kuwa mambo yatakuwa mazuri kwa muda mfupi.
Mashabiki wanataka uaminifu na uwazi,” alisema beki huyo wa kati wa zamani wa Barca akikiambia kituo cha Twitch cha Tbai Llanos.
“Kama ukweli ni mgumu, waseme kuwaambia kwamba, hatutashinda Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa huna fedha za kushindana ni uongo.”
“Sijui hali ya klabu kwa sasa kutokana na kile ninachoweza kukusanya haionekani kuwa nzuri lakini kile wanacho thamini jamii (wanachama) ni kuambiwa ukweli kwenye nyuso zao.”
Moja kubwa chanya kwa Barca msimu huu ni kuibuka kwa vijana wenye vipaji kama Lamine Yamal, Pau Cubarsi na Fermin Lopez kutoka akademi yao.
Pique, ambaye alistaafu mwishoni mwa 2022, anaamini mashabiki wataelewa ikiwa Rais Joan Laporta atasema klabu hiyo itazingatia wachezaji wa nyumbani huku ikirejea katika hali ya kifedha.
“Ukisema, tazama, hatuna hata senti ya kutumia, kwa hiyo miaka miwili au mitatu ijayo tutageukia La Masia,’ watu watakubali,” alisema.
“Ujumbe unapaswa kuwa kwamba tuna imani na akademi, kwamba kuna wachezaji wazuri na wenye vipaji vingi. Walete na ujaribu kushindana kwenye La Liga.”