Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha ameondoka nchini leo Alhamis (Machi 07) kuelekea kwao Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi ya siku tano itakayofanyika nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Simba kupitia kwa Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally imeeleza kuwa akiwa Algeria Benchikha atazikosa mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo ni dhidi ya Coastal Union na Singida Fountain Gate zitakazochezwa Machi 9 na 12.
Katika kipindi hicho Benchikha amemuachia mikoba msaidizi wake, Farid Zemiti akishirikiana na Benchi lake la Ufundi kukiongoza kikosi hicho.
Jana Jumatano (Machi 06) Benchikha alishuhudia kikosi chake kikiadhibiwa na Tanzania Prisons kwa kuchapwa 2-1 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.