Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI – Dkt. Rashid Mfaume ameuelekeza uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi mashine zilizopo jengo la kufulia zianze kutumika.
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo akiwa ameambatana na timu ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mkoani Katavi kwa ajili kukagua miradi ya Afya na kufuatilia ufanisi na utendaji wa watoa huduma za Afya na wamebaini vifaa vilivyoletwa katika hospitali hiyo ikiwemo mashine ya kufulia nguo na kukausha pamoja na pasi vimekaa zaidi ya mwaka mmoja bila kutumika.
Amesema, “Mashine hii ya kufulia imepokelewa zaidi ya mwaka mmoja lakini kunamashine ya kukaushia nguo tumeiona na ‘stand by generator’ lakini watumishi wa hapa kwa taarifa tulizonazo wanafua kwa kutumia mikono.
Aidha, ameongeza kuwa, “tumeona mabeseni hapa wakati mama Samia alikuwa na nia ya dhati ya kuwasaidia watendaji na ukiangalia thamani ya vifaa ni kubwa mno kuvileta na kuviweka kwenye eneo kama hili haipendezi na wala haifurahishi na Rais Samia hafurahishwi na jambo kama hili na kila kiongozi hatofurahishwa na kitu kama hiki.”

Kikao cha maridhiano sakata kitita kipya NHIF ni jumatatu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji avunja ukimya siku ya Wanawake