Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amehudhuria hafla ya The Citizen Rising katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika hafla hiyo amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo namna ambavyo alisikia minong’ono, kujiuliza ni namna gani na jinsi alivyoweza kushughulikia suala la kuiunganisha nchi na hapa ni baadhi ya nukuu zake muhimu akiwa katika ukumbi huo.

Amesema, “nilijiuliza kwanini watu wanasema Mama unganisha taifa, kuna nini? Wapi taifa limegawana? Kwahiyo, nikafanya kazi ya kusoma ile hali ilivyo nikasema sasa nadhani tunahitaji kuwa na falsafa ambayo si Serikali peke yetu lakini vyama vya siasa na wengine tunaweza kuitumia hiyo falsafa na tukaweza kuliunganisha taifa na tukaenda mbele.”

Ameongeza kuwa, “akili ni vile unavyozitumia, mwanadamu yeyote aliyeumbwa na Mungu ana karama Mungu amempa, inategemea makuzi yanavyoendelezwa na anavyoona mambo, kwa hiyo, nataka niseme; tusidharauliane, kila mwanadamu akijengewa uwezo anaweza kufanya chochote kile.”

“Nchi ikiwa na amani na utulivu, Mwenyezi Mungu anashusha baraka ya kila jambo. Kwahiyo niwaombe sana watu tuendelee kuweka utulivu na amani katika chaguzi zetu hizi. Ushindani ufanywe kwa halali, tuweke amani na utulivu ili Mungu naye atushushie baraka zake tupate viongozi wema,” alisema Rais Samia.

Ukatili: Jamii ya Kimasai yaonywa
Dkt. Mwinyi: Misikiti itumike kutatua changamoto za jamii