Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amevipongeza Vikosi vya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Zimamoto na Uokozi na Chuo cha Mafunzo kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo Madarasa, Masoko na Vituo vya Wajasiriamali.

Dkt. Mwinyi ametoa pongezi hizo wakati  akizungumza na Maafisa na Wapiganaji alipowatembelea Vikosi vya Zimamoto na Uokozi, JKU na Chuo cha Mafunzo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ.

Aidha, amewahimiza umuhimu wa nidhamu, uzalendo, uadilifu na umoja kwa Maafisa na Wapiganaji hao wazalendo.

Rais Dkt. Mwinyi pia amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar0 itaendelea kuboresha miundombinu ya Vikosi hivyo.

Watoa wito kusitisha mapigano mwezi Mtukufu
Kazungu jela maisha kwa mauaji ya Watu 14