Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Rashid Mfaume amezielekeza timu za usimamizi wa huduma za Afya Ustawi wa jamii na Lishe ngazi ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri (CHMT), kusimamia thamani ya fedha za ujenzi wa miradi ya Afya inayojengwa katika maeneo hayo.

Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara ta timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka ofisi ya Rais – TAMISEMI ya usimamizi shirikishi na ufanisi wa utoaji huduma katika mkoa wa katavi ambapo timu hiyo imebaini kuwa timu hizo hazina ufahamu wa gharama za kila jengo lililojengwa katika Hospitali za wilaya,Vituo vya Afya na Zahanati.

Amesema, “Hatuko vizuri sana katika kufuatilia makisio ya gharama za ujenzi wa miradi ya Afya matumizi ya fedha kwa kila jengo kama Hospitali inamajengo 14 tunataka kila jengo kufahamu limetumia shilingi ngapi katika maeneo ambayo tumepita sababu tulizozipata hazikubaliki kwa hiyo mkafanye hiyo kazi kwa kushirikiana na ma- engineer na wakadiria majengo tunataka kila jengo katika miradi yote iwe ni Hospitali,Kituo cha Afya na Zahanati tujue gharama kuu na iwe inegawanywa kwa gharama ndogondogo kwa kila jengo haya ni maelekezo kwa halmashauri zote.”

Akizungumzia suala la vifaa tiba vinavyoweza pelekwa kwenye maeneo ya kutolea huduma za Afya,Dkt. Mfaume ameelekeza vifaa hivyo ikiwemo vifaa katika jengo la kufulia vinatakiwa kufungwa na kuanza kutoa huduma badala kuviacha vikae kwa muda mrefu.

Miguel Gamondi: Kisasi kitalipwa
Wezi wa Maboya Kivuko cha Kigamboni waonywa