Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wananchi wa Kata ya Maiska B iliyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara, wametakiwa kudumisha ulinzi na usalama katika maeneo yao ili kuondoa uhalifu na vitendo vya kikatili katika Jamii.

Hayo yamesema na Mlezi wa Vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi vya kata ya Babati Mkuu wa Kituo cha Polisi Babati, OCS. Amiri Mlemba wakati wa hafla ya kutimiza miaka miwili ya kikundi hicho cha maisaka B.

Naye mwenyekiti wa kikundi hicho, Benard Raphael amesema lengo la kikundi hicho ni kudhibiti vitendo vyote vya kikatili ikiwemo ubakaji,uporaji,matumizi ya pombe haramu aina ya gongo na matumizi ya dawa za kulevya katika Jamii na kuziomba mamlaka mbalimbli kuweza kuvisaidia vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi Ili kuwatia moyo zaidi wa kulinda mitaa Yao.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ACP Sweetbertue Mkoyi, amekipongeza kikundi hicho Kwa kukabiliana na uhalifu katika Kata na mitaa na amehadi kuwaongezea nguvu Zaid Ili kuleta ufanisi ,pamoja na kuboresha kikundi hicho na vikundi vingine katika kata ya Babati.

Xabi Alonso asubiriwa Real Madrid
Pascal Wawa ageukia ukocha