Afisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la Serikali Nchini Sudan, Jenerali Yasser al-Atta, amesema hakutakuwa na usitishaji wa mapigano wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadan.

Yasser amesema, makabiliano ya kivita yataendelea hadi pale wapiganaji wa kikundi cha akiba – RSF, watakapoondoka kwenye maeneo ya raia.

Tamko hilo, limekuja kufuatia wito wa Baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa vita kupisha mwezi mtukufu.

OSHA wakamilisha tathmini vihatarishi vya usalama, afya JNHPP
Teuzi tisa za Rais Samia, watatu wahamishwa