Lydia Mollel-Morogoro.

Watumiaji wa Barabara ya  Mikumi – Kilombero  Mkoani Morogoro wamelazimika kukaa zaidi ya saa  kumi 12 Barabarani baada Bimu ya Daraja la Muzombe 12 kupinda na kusababisha magari kushindwa kupita.

Msimamizi kitengo cha matengenezo ya Barabara na Madaraja wa TANROADS, Mhandisi Patrick Rambika amesema changamoto hiyo ilitokea baada ya Mvua kubwa iliyopelekea kufurika kwa maji.

Amesema, tijihada za haraka za kurudisha mawasiliano katika eneo hilo zinaendelea na Magari yataruhusiiwa kupita mara baada ya matengenezo yatakayofanyika kwa zaidi ya saa 4 hadi 5.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ally Mussa amewaondolea hofu watumiaji wa barabara na kusema Serikali ipo kazini kuhakikisha huduma hiyo muhimu ya usafiri na usafirishaji inarejea kwa wakati.

Julio anasubiri muda Singida FG
AngloGold Ashanti yamuahidi Rais Samia kuwawezesha Wanawake sekta ya Madini