Kiungo wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Joshua Kimmich amesisitiza kuwa hana haraka juu ya mustakabali wake klabuni hapo, lakini bado hajafanya mazungumzo kuhusu hali ya mkataba wake mpya.

Kimmich ameingia miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake na amekuwa akihusishwa na kuhamia Ligi Kuu ya England, ambapo miamba kama Manchester United, Manchester City na Liverpool zote zimetajwa kuwa na nia ya kumsajili.

“Kwa ujumla, hali yangu iko wazi,” alisema Kimmich baada ya ushindi wa Bayern wa 8-1 dhidi ya Mainz mwishoni mwa juma lililopita.

“Bado nina zaidi ya mwaka mmoja kwenye mkataba wangu. Hakuna mtu ambaye amezungumza nami. Ndiyo maana nimepumzika sana.

“Hebu tuone nini kitatokea. Kwangu, jambo muhimu zaidi ni kwamba ninafanya vizuri, kwamba nifikie uchezaji wangu wa juu, na siwezi kushawishi wengine.”

Mustakabali wa Kimmich pia uliwekwa kwa Mkurugenzi wa Bayern, Max Eberl, ambaye alikiri klabu hiyo inahitaji kujua ni nani atakuwa kocha wao ajaye kabla ya kufanya uamuzi kuhusu hali ya mkataba wa Kimmich.

“Ni mchezaji muhimu sana na anayestahili Bayern Munich,” alisema Eberl akiiambia Sky Sports.

“Pia itategemea na kocha mpya na jinsi atakavyomwona Josh. Kwa sasa anahitajika kwenye safu ya ulinzi, ambapo anafanya vizuri sana na ni msaada mkubwa kwetu. Lakini pia Josh ni mchezaji wa nafasi ya kiungo.

“Lakini nadhani kocha mpya anaweza kuwa na maoni tofauti na kumwona mchezaji kwa njia tofauti. Kimsingi tunapaswa kusubiri na kuona.”

Magari, Pikipiki vyakabidhiwa kuendeleza Kilimo, Uvuvi
PSG yamtengea mabilioni Lamine Yamal